Published On: Tue, Apr 10th, 2018
Business | Post by jerome

Wawekezaji kwenye viwanda vya dawa nchini wakosa mitaji

Share This
Tags

Wakati ripoti ya wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa nchini ikitarajiwa kufikishwa katika Baraza la Mawaziri wiki hii, imebainika kuwa zaidi ya wawekezaji 30 waliojitokeza wana ujuzi, ardhi na mawazo lakini hawana mitaji.

Wawekezaji 38 walipatikana baada ya kikao cha Aprili 4 kati ya wafanyabishara hao na Serikali, huku Aprili 5 kikifanyika kikao cha ndani baina yao na wengine 30 wenye ujuzi waliojitokeza.

Suala hilo limekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kukaribisha wawekezaji kujenga viwanda vya dawa kukabiliana na upungufu uliopo katika sekta hiyo, wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya Dawa (MSD), Machi 26.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kwa sasa wizara yake na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji zimekamilisha kazi ya awali na kuandaa ripoti itakayopelekwa Baraza la Mawaziri.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>