Published On: Wed, Apr 11th, 2018
World | Post by jerome

Watu zaidi ya 100 wafariki baada ya ndege ya kijeshi kuanguka Algeria

Share This
Tags

Maafisa wanasema karibu watu 100 wamefariki dunia leo kufuatia ndege moja ya kijeshi kuanguka muda katika shamba moja muda mfupi baada ya kupaa kaskazini mwa Algeria.

Taarifa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi inasema chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijajulikana na kwamba uchunguzi unafanyika. Vikosi vya huduma za dharura zilifika katika eneo la tukio ambalo ni karibu na kambi ya kijeshi ya Boufarik.

Msemaji wa shirika la ulinzi wa raia, Mohammed Achour, amesema waliofariki ni zaidi ya mia moja na ndege hiyo ilikuwa imewabeba wanajeshi. Wizara ya Ulinzi haikutoa idadi kamili ya walioaga dunia ila imetoa rambi rambi kwa familia za waaliofariki.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>