Published On: Mon, Apr 16th, 2018

WATU TISA WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NCHINI

Share This
Tags

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limethibitisha kutokea vifo tisa vya watu vilivyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Jiji hilo limejaa maji katika maeneo mengi na kusababisha wengine kukosa makazi.

Baadhi ya maeneo yaliyolemewa na mafuriko ni Mnyamani, bonde la Mpunga, Kigogo, Mikocheni, Vingunguti, Tabata Kisiwani na Kurasini.

Maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko, maji yamefika pia.

Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika baadhi ya barabara na madaraja ya na kusababisha kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Wananchi wameendelea kuhimizwa kuondoka katika maeneo hatarishi ili kuyanusuru maisha yao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>