Published On: Tue, Apr 17th, 2018

Wataalam wa Malaria wakutana Senegal

Share This
Tags

Wanasayansi wapatao elfu tatu wanakutana nchini Senegal katika mkutano wa saba wa kimataifa wa afya kujadiliana juu ya ugonjwa wa malaria kwa siku tano mfululizo wiki hii.

Ni miaka 20 sasa tangu mkutano wa kwanza wa kimataifa ulifanyika, ambao pia ulikuwa nchini Senegal.

Wakati huo, hapakuwa na matarajio mengi ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huo unaoletwa na vimelea vinavyosababishwa na mbu.

Sasa Shirika la Afya duniani linaamini kuwa nchi sita barani Afrika wanauwezo mkubwa wa kuutokomeza kabisa ugonjwa huo – Algeria, the Comoros, Madagascar, The Gambia, Zimbabwe and Senegal.

Senegal imepiga hatua kubwa sana , ikirekodi kuwa na upungufu wa vifo wa asilimia 40 ndani ya miaka 10 iliyopita.

Lakini hatua hizo bila shaka zimekutana na changamoto.

Malaria inapatikana katika nchi 91 duniani, lakini idadi kubwa ya vifo hutokea katika nchi 18.

Pia idadi ya vifo imeongeka katika nchi za Nigeria, Ivory Coast, South Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Shirika la Afya duniani inasema watu 4000,000 wanafariki kila mwaka kwa sababu ya ugonjwa wa malaria . Wengi wao ni watoto.

Serikali ya Senegal imeanzisha matibabu ya bure kwa watoto waliochini ya umria ya miaka mitano. Dawa zimeboreshwa. Lakini mabadiliko makubwa yametokea katika kiwango cha uelewa wa jamii na juhudi zao katika usafi.

Doudou Sene, ni mratibu wa programu wa taifa ya vita dhidi ya malaria – programu hio ya serikali imesaidia nchi ya Senegal kupiga hatua kubwa katika kutokeomeza vimelea vinavyosababishwa na mbu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>