Published On: Mon, Apr 16th, 2018

UPUNGUFU WA WALIMU KUISHA HADI KUFIKIA 2020

Share This
Tags

Serikali imesema hadi kufika 2020 tatizo la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi litakuwa limekwisha huku ikiwataka wananchi kujitolea kushiriki katika ujenzi wa maabara katika shule zao.

Naibu waziri wa TAMISEMI, JOSEPH KAKUNDA ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mchinga HAMIDU BOBALI aliyeuliza ni lini serikali itamaliza changamoto ya ukosefu wa walimu wa sayansi na vyumba vya maabara.

KAKUNDA amesema mpango wa sasa ni kuajiri walimu 6,000 hadi June 30 mwaka huu na kusema serikali haijakataza michango mashuleni ya kuchangia miundombini bali kilichokatazwa ni wanafunzi kufukuzwa shule kisa mzazi hajatoa mchango.

Katika hatua nyingine serikali imesema matumizi ya dola nchini sio sababu ya shilingi kushuka thamani bali vihatarishi vya hali hiyo ni mfumuko wa bei na tofauti ya misimu.

Naibu waziri wa fedha na mipago DK. ASHATU KIJAJI ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum DEVOTHA MINJA aliyeuliza ni lini serikali itarekebisha sheria ili kuzuia matumizi ya dola nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>