Published On: Thu, Apr 12th, 2018

UMOJA WA MATAIFA WAAHIDI KUSAIDIA TEKNOLOJIA YA KISASA KWA VIJANA KIGOMA

Share This
Tags

Shirika la Umoja wa Mataifa, UN, kupitia program ya pamoja ya Kigoma (Kigoma Joint Program), limeahidi kusaidia upatikanaji wa teknolojia ya kisasa kwa vijana wajasiriamali wanaofanya shughuli za uzalishaji mali ili waweze kuboresha Maisha yao

Mkurugenzi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini Alvaro Rodriguez, amesema alipotembelea Mradi wa Kiwanda kidogo cha utengenezaji wa Sabuni kwa kutumia mafuta yanayotokana na zao la Michikichi.

Kiwanda hicho kinaendeshwa na Mmoja wa Vijana waliopewa Mafunzo ya ujasiriamali kupitia moja ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, ILO ambalo ni Shirika la kazi Duniani

Mkurugenzi huyo, amesema Mradi huo wa Vijana ni mfano mzuri wa namna Vijana wanavyoweza kutumia nguvu zao na Rasilimali zinazowazunguka kutengeneza fursa za Ajira na kipato kwa manufaa ya watu wa Kigoma, lakini bado wanatumia teknolojia duni.

Tayari Vijana 57 wamepata Mafunzo ya ujasiriamali wa nadharia na vitendo kupitia ufadhili wa Shilingi Milioni 67 kutoka Shirika la Kazi Duniani, ILO.

Serikali Mkoani humo imetoa wito kwa Vijana kujiunga katika Vikundi mbalimbali ili waweze kupata Mikopo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>