Published On: Mon, Apr 16th, 2018

UJENZI WA BARABARA YA BUNJU B

Share This
Tags

Serikali imesema Ujenzi wa Barabara ya Bunju B Kupitia Mpiji Magohe, Kifuru hadi Pugu Kiltex yenye urefu wa kilomita 33.7 inayopita kwenye jimbo la kibamba jijini Dar es Salaam, utaanza mara baada ya usanifu kukamilika na fedha za ujenzi kupatikana.

Mnamo mwaka 2010 serikali ilianza mpango wa kukabiliana na tatizo la msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa kutekeleza mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara za pete na zile za mchepuo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ELIAS KWANDIKWA ameyazungumza hayo Bungeni Mjini Dodoma.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuo kuanzia tangi bovu hadi kinyerezi kupitia Goba, Mbezi Mwisho na Malambamawili, Waziri KWANDIKWA  amesema utekelezaji wake utaanza.

Wakati huo huo naibu waziri wa maji na umwagiliaji JUMAA AWESO, amesema utekelezaji wa awamu ya kwanza na pili ya programu ya maendeleo ya sekta ya maji, serikali imetekeleza miradi katika vijiji 230 kwenye mkoa wa Ruvuma.

Akijibu swali la mbunge wa viti maalum SIKUDHANI CHIKAMBO, Naibu Waziri AWESO amesema, katika Mwaka wa Fedha 2017/2018, mkoa huo ulitengewa shilingi bilioni 18.44, kwa ajili ya kukamilisha ujenzi, ukarabati, usanifu, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>