Uganda yapiga marufuku uuzaji wa mkaa Kenya
Serikali ya Uganda imepiga marufuku uuzaji wa mkaa kwenda Kenya katika juhudi za kulinda misitu nchini humo.
Kamishna wa wilaya ya Busia Uganda, Hussein Kato Matanda, ametangaza kwenye eneo la mpakani kwamba sasa uuzaji wa mkaa ni kinyume cha sheria.
Awali Kenya imeweka marufuku ya ukataji miti na uuzaji wa mkaa baada ya kubaini kuwa misitu mingi imeangamia kutokana na shughuli hizo.
Kutokana na marufuku ya Kenya wadau wa mkaa nchini Uganda wamekuwa na soko zuri, huku gunia moja likapanda bei maradufu hadi dola 22 kutoka bei ya awali ya dola 10.