Published On: Tue, Apr 17th, 2018

Serikali yatambua umuhimu wa Diaspora

Share This
Tags

Serikali imekiri Kutambua Umuhimu wa Diaspora Katika Kuleta  Manedeleo Nchini, Kupitia Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano Kuelekea Uchumi wa Kati.

Akijibu Swali la Mbunge wa Welezo, SAADA MKUYA, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Elimu WILLIAM OLE NASHA, amesema Diaspora ni Wadau Muhimu Katika Suala la Maendeleo.

Naibu Waziri huyo wa Elimu ameongeza Kuwa Watanzania Waishio Nje ya Nchi, wamekuwa wakichangia Ukuaji wa Uchumi Kupitia Uwekezaji Kwenye Sekta Mbali mbali ikiwemo Biashara, Afya na Elimu.

Katika hatua Nyingine Bunge Limeelezwa Serikali Kupitia Mahakama inazo Kumbukumbu na Taarifa za Wananchi Wanaolipa Faini na Baadae Kushinda Rufaa za Kesi Zao.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa PALAMAGAMBA KABUDI ametoa Kauli hiyo Wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Rombo, JOSEPH SELASINI.

 

Bunge la Bajeti linaendelea Dodoma, ambapo Mjadala Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Unaendelea.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>