Published On: Wed, Apr 11th, 2018
Sports | Post by jerome

Serikali yaahidi kuendelea Kuimarisha Mchezo wa Soka

Share This
Tags

Naibu Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo JULIANA SHONZA amesema Serikali itaendelea Kuimarisha Mchezo wa Soka kwa Kusimamia Programu mbalimbali zinazoanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.

Amesema ili kufikia Dhamira ya Kuinua Mchezo huo, Shirikisho la Mpira TFF lipo Kwenye Programu ya Uboreshaji wa Viwanja vya Soka Ukiwemo Ule wa Nyamagana na Kaitaba Mkoani Kagera.

Kuhusu Mapato ya TFF, Naibu Waziri SHONZA amelieleza Bunge kuwa Shirikisho hilo la Mpira wa Miguu lina udhamini wa Miaka Minne Kutoka FIFA kupitia Programu ya FIFA Forward, pamoja na Mikataba Mingine kwa ajili ya Taifa Stars na Ligi Kuu ya Wanawake.

Wakati huo huo Bunge limemteua Mbunge wa Viti maalum AMINA MOLLEL kuwa Msemaji rasmi wa Klabu ya Bunge Sports.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>