Published On: Tue, Apr 10th, 2018

Serikali itaendelea kuzichukulia hatua kazi za sanaa zinazokiuka maadili

Share This
Tags

Serikali imesema itaendelea kuzichukulia hatua kazi za sanaa ikiwa ni pamoja na nyimbo za wasanii zinazokiuka maadili ili kulinda utamaduni na maadili ya mtanzania.

Hayo yamesemwa na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu mkoa wa Arusha Catherine Magige (CCM) aliyetaka kujua ni kwa nini siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa kufungiwa kwa nyimbo na wasanii.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa  kila taifa lina utamaduni wake na ni lazima liulinde kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanywa na serikali siyo vita dhidi ya wasanii bali ni kuhakikisha kuwa serikali inalinda maadili ambayo katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolijia ya habari na mawasiliano  kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili hapa nchini, hivyo serikali ni lazima ichukue hatua.

Amefafanua kuwa, kinachofanyika hivi sasa hapa nchini ikiwemo kufungia nyimbo za wasanii siyo jambo geni kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikiwachukulia hatua za kinidhamu wasanii wao wanapokiuka maadili na utamaduni wa nchi hizo.

Akitoa mfano kwa nchi ya Marekani, Dkt. Mwakyembe amesema mwanamuziki RICK ROSS wiki chache zilizopita amepata matatizo kwa kutoa wimbo ambao maudhui yake yanajenga picha  ya kwamba anaunga mkono ubakaji, kitendo kilichopelekea nyimbo hiyo kufungiwa mara moja na yeye kuomba radhi”

Aidha, Dkt. Mwakyembe amewataka wabunge kuiunga mkono serikali katika kulinda utamaduni wa mtanzania kwani yanayotokea Tanzania yanatokea duniani kote.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>