Published On: Tue, Apr 10th, 2018

Nyanya na tufaha zawasaidia wanaoacha uvutaji wa sigara kurekebisha uwezo wa mapafu

Share This
Tags

Utafiti mpya umeonesha kuwa baada ya kuacha kuvuta sigara, ulaji wa nyanya bichi na tufaha unaweza kusaidia kurekebisha uwezo wa mapafu.

Katika utafiti unaofanyika kwa miaka kumi, watafiti wamefanya upimaji wa uwezo wa mapafu na uchunguzi wa chakula kati ya watu zaidi ya 650 kutoka Ujerumani, Norway na Uingereza. Matokeo yameonesha kuwa, baada ya kuacha uvutaji wa sigara, ulaji wa nyanya na tufaha unaweza kupunguza hasara kwa mapafu.

Kwa kulinganishwa na watu wanaokula nyanya isiyozidi moja au matunda kwa siku, watu wanaokula nyanya zaidi ya mbili au matunda matatu, uwezo wa mapafu unaweza kupungua kwa kasi ndogo.

Utafiti umeonesha kuwa chakula hicho kinaweza kusaidia kurekebisha hasara zinazotokana na uvutaji wa sigara. Wamesisitiza kuwa njia ya kula ni muhimu sana, ulaji wa nyanya na matunda bichi unaweza kulinda mapafu, lakini nyanya au matunda kutoka vyakula vingine hazitatoa mchango kama huo.

Wakati huohuo, pia wamegundua kuwa ulaji wa nyanya bichi unaweza kutoa mchango wa kidhahiri zaidi kwenye mwili wa wale waliokuwa wavutaji wa sigara.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>