Published On: Mon, Apr 16th, 2018

MWENYEKITI WA CHADEMA MANISPAA YA MOROGORO ASIMAMISHWA UANACHAMA KWA TUHUMA ZA UTAPELI

Share This
Tags

Baraza  kuu  la uongozi  wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo CHADEMA  Mkoa wa Morogoro  limemvua   uongozi aliyekuwa    Mwenyekiti wa Chama    manispaa ya Morogoro JAMES MKUDE  kutokana na madai ya   kuhusishwa  na   tuhuma mbalimbali ikiwemo utapeli.

Akitoa maazimio ya baraza hilo mwenyekiti wa chama hicho  Mkoa wa  Morogoro ambaye pia  ni mbunge wa jimbo la  Mlimba     SUZAN  KIWANGA   amesema  kwa mujibu wa katiba ya chama hicho   ya mwaka 2006  toleo la mwaka 2016  kifungu cha saba  kinatoa  mamlaka  kwa baraza  kuu la  uongozi  kumsimamisha   uongozi  mtu yeyote atakaekiuka  maadili ya kinidhamu ya chama hicho.

Mwenyekiti huyo amesema MKUDE anatuhumiwa kufanya utapeli huko jijini Arusha,  hata hivyo hakuweka wazi kuwa ni kiasi gani    cha fedha alichotapeli.

Akizungumza kwa njia ya Simu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP ULRICH MATEI amesema kuwa walipata taarifa ya JAMES MKUDE kutafutwa  na Polisi mkoa wa Kilimanjaro  kwa madai ya kuhusishwa kwenye utapeli wa shilingi milioni mia nne baada ya kudai kuwa yeye na wenzake wangeweza kumfufua mtoto wa mama mmoja Mkazi wa Majengo mkoani Kilimanjaro iwapo watapatiwa kiasi hicho cha fedha.

JAMES MKUDE kwa sasa ameshapelekwa mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na askari polisi wa Mkoani humo kwa kushirikiana na askari wa mkoa wa Morogoro.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>