Published On: Thu, Apr 12th, 2018
World | Post by jerome

MWANAMKE WA RWANDA AWEKWA KWENYE ORODHA YA WANAWAKE MASHUHURI

Share This
Tags

Mwanaharakati wa masuala ya Wanawake nchini Rwanda Godelive Mukasarasi amewekwa kwenye orodha ya wanawake 10 mashuhuri duniani.

Tuzo aliyopewa na Marekani Bi Godelive Mukasarasi inatokana na jhudi za shirika aliloanzisha nchini Rwanda la SEVOTA kusaidia wakinamama walionusurika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Amewekwa kwenye orodha hiyo na nchi ya Marekani ambao hivi karibuni walitunukiwa tuzo ijulikanayo kwa jina”International women of Courage ” kutokana na shughuli za shirika lake la SEVOTA ambalo husaidia wanawake waliobakwa wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda pamoja na watoto waliozaliwa kutokana na kitendo hicho.

Shirika hilo limekuwa likisaidia wakinamama hao kujijenga kimaisha, kupokea yaliyowapata na kuwapa upendo watoto waliozaa kwa namna hiyo.

Shirika hilo aliloanzisha limeweza kukusanya watu wasiopungua elfu 10 ambao ni wanawake wajane wa mauaji ya kimbari na watoto yatima.

Kadhalika tuzo aliyopewa ni baada ya kile kilichotajwa kuwa juhudi zake kupigania kosa la ubakaji kuwa miongoni mwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>