Published On: Wed, Apr 4th, 2018
Sports | Post by jerome

Michuano ya mpira wa nyavu ya wanawake klabu bingwa Afrika: Al Ahly yatwaa ubingwa

Share This
Tags

Michuano ya mpira wa wavu (Volleyball) kwa wanawake imemalizika huku timu ya wanawake ya mpira wa wavu ya Al Ahly ikiibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya kuifungashia virago timu ya wanawake ya Tunisia kwa seti 3-0 katika mchezo wa fainali iliyochezwa kwenye ukumbi wa Al Ahly mjini Cairo Misri.

Timu ya wanawake ya Pipeline toka Kenya ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuwashinda ndugu zao wa Kenya, Prisons seti 3-0 katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu.

Fainali za michuano hiyo kwa wanaume zitafanyika kesho mjini Cairo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>