Published On: Tue, Apr 17th, 2018

Mgogoro kati ya serikali na familia ya chifu Mkwawa watatuliwa.

Share This
Tags

Wizara ya maliasili na utalii imetatua mgogoro uliohusu umiliki wa Makumbusho ya chifu Mkwawa iliyopo kijiji cha kalenga baina ya serikali ya mkoa wa Iringa na familia wanaodai kutonufaika na uwepo wa makumbusho hayo.

Utatuzi wa mgogoro  huo umefikiwa ikiwa ni siku chache tangu ifanyike ziara ya waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na michezo kama sehemu ya kuendeleza mali kale na kupata malalamiko ya familia ya Mkwawa kutoridhishwa na usimamizi wa makumbusho hayo.

Saa sita zimetumika katika kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro chini ya Katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Mstaafu Gaudence Milanzi na baadae akatoa neno kuashiria kumalizika kwa mgogoro huo huku akiahidi serikali kutekeleza miongoni mwa mambo yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Suala la ushirikiano katika usimamizi wa Makumbusho hayo baina ya serikali na familia ndilo linalopewa kipaumbele ili kuhakikisha pande zote mbili zinaridhia ili kuondoa tofauti zilizokuwepo awali.

Na hatimaye familia ya Chifu Mkwawa ikatoa neno namna walivyopokea maridhiano hayo na kuiomba serikali kutekeleza kwa vitendo makubaliano hayo ili kuhakikisha mila na desturi ya familia hiyo inaendelezwa.

Mgogoro huo umedumu kwa miongo kadhaa sasa huku familia hiyo ikitishia kuifunga makumbusho hayo pamoja na kuifikisha serikali mahakamani kwa kile kinachoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa mila na desturi za kabila la wahehe jambo linaloweza kuwa na athari katika familia hiyo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>