Published On: Tue, Apr 17th, 2018
Sports | Post by jerome

Mashindano ya Vijana Burundi: Zanzibar yafungiwa kwa madai ya kupeleka vijana waliozidi umri

Share This
Tags

Michuano ya Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA Challenge Cup U-17) inayofanyika nchini Burundi imeendelea jana ambapo Uganda na Tanzania Bara, zilicheza na kutoka sare ya magoli 1-1.

Katika hatua nyingine, Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar, Karume Boys imefungiwa kutoshiriki mashindano ya CECAFA kwa kile kilichodaiwa kuwa wamepeleka wachezaji waliozidi umri kwenye michuano ya Burundi.

Pamoja na adhabu hiyo, CECAFA Pia imeitoza timu hiyo faini ya dola za kimarekani 15,000 kwa kosa hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>