Published On: Tue, Apr 17th, 2018

Makamu wa rais akutana na Prince William jijini London

Share This
Tags
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la Buckingham Palace.

Makamu wa Rais amemweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado hatujawa na teknolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.

Kwa upande wake Prince Williams amemuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na pia Prince William amemualika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.

Makamu wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.‚Äč

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>