Published On: Tue, Apr 10th, 2018
Sports | Post by jerome

Leverkusen yaiadhibu RB Leipzig katika Bundesliga

Share This
Tags

Bayer Levekusen ilitoka nyuma na kuichabanga RB Leipzig mabao manne kwa moja katika mchuano mkali wa ligi kuu ya kandanda Ujerumani – Bundesliga, na kuwapiku wapinzani wao hao katika nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ushindi huo umewaweka Leverkusen katika nafasi ya nne, na pointi 48, mbele ya Leipzig ambao wameteremka hadi nafasi ya sita na pointi 46 nyuma ya Eintracht Frankfurt kwa tofauti ya mabao. Timu nne za kwanza zitafuzu katika hatua ya makundi ya Champions League msimu ujao.

Wakati huo huo, timu mbili za kwanza kutinga katika nusu fainali ya Champions League zitajulikana leo. Manchester City itahitaji kutoka nyuma na kukifuta kichapo cha tatu bila wakati watakapowaalika Liverpool katika mchuano mkali wa mkondo wa pili wa robo fainali.

Nao AS Roma wa Italia watawaalika Barcelona huku Waitaliano hao wakiwa na mlima mkubwa wa kukwea kama watataka kutinga katika nne ya mwisho kwa mara yao ya kwanza tangu mwaka wa 1984. Roma walirambishwa mabao manne kwa moja na Barca katika mkondo wa kwanza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>