Published On: Tue, Apr 17th, 2018

Kwa nini Saratani nyingine ni ‘hatari’

Share This
Tags

Utafiti umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani ingawa zinaonekana kufanana

Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake

Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ”ni hatari” huku nyingine zikiwa hazina madhara na wakati mwingine hazihitaji matibabu

Taasisi ya utafiti la Cancer Research ya Uingereza imesema utafiti huu unasaidia wagonjwa kupata uangalizi mzuri wa kitabibu

hatuwezi kutofautisha kati ya unaohitaji tiba na usiohitaji.

Mtu mmoja mwenye saratani anaweza kufa haraka kuliko mtu mwingine mwenye saratani inayofanana ambaye anaweza kuishi kwa miongo kadhaa baada ya matibabu

Kazi iliyochapwa kwenye jarida liitwalo Journal Cell, iliainisha saratani za figo kwa wagonjwa 100

Wakati saratani ikikua zinakuwa zikibadilika zaidi na hatimae sehemu mbalimbali za uvimbe zinajiunda kwa namna mbalimbali

Watafiti huchukua sampuli kutoka sehemu mbalimbali za uvimbe huohuo na kutazama kwa namna gani zina uhusiano wa karibu

Michael Malley, 72,kutoka London, alishiriki kufanyiwa vipimo hilo kwenye hospitali ya Royal Marsden baada ya kugundulikwa kuwa na saratani ya figo.

Alisema: ”kwa kweli tafiti kama hizi ni muhimu kwa ajili ya kupata uelewa ni jinsi gani saratani ya figo inavyokua kadiri muda unavyokwenda, na nina matumaini kuwa hii itasaidia wagonjwa kama mimi kupata tiba nzuri.

bado kuna changamoto ya namna nzuri ya kutibu kila aina ya uvimbe, pia namna ya kufanya uchunguzi kwenye hospitali badala ya maabara za utafiti

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>