Published On: Wed, Apr 11th, 2018
Business | Post by jerome

Kushuka kwa bei ya unga,nafuu kwa gharama za nyumba

Share This
Tags

Bei ya unga wa mahindi Nchini Kenya imeshuka zaidi kufuatia kufuatia kupungzwa kwa asilimia 10 ya gharama ya mahindi kabla ya kupelekwa kwa wasagaji wa bidhaa hiyo.

Gunia la mahindi wa wasagaji wa mahindi kwa sasa linauzwa kwa Sh1,100 kutoka kiwango cha bei ya Sh1,230 ya mwezi Januari mwaka huu, huku wasagaji wa mahindi wakihusisha punguzo hilo la bei na kushuka kwa bei ya mahindi kwenye masoko.

Kupungua kwa bei ya gunia la mahindi kuliwafanya kumewafanya baadhi ya wauzaji wa jumla kuuza mfuko wa kilo mbili wa unga kwa Sh100 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Tangu mpango wa ruzuku kwa mauzo ya unga ulipomalizika mwishoni mwa mwezi wa Disemba mwaka jana, bei ya unga wa ugali ilipanda hadi kufikia Sh115 kutoka Sh90 huku wasagaji wa mahindi wakilaumu ughali wa bidhaa hiyo sokoni.

Lakini kwa sasa wasagaji wa mahindi wananunua mfuko wa kilo 90 za mahindi kwa Sh2,300 kutoka kiwango cha Sh3,000 cha mwezi wa in Disemba.

Mfuko wa kilo mbili wa nembo ya Jimbi unauzwa kwa Sh98 kutoka Sh101, Kifaru Sh99 kutoka Sh104, Soko Sh100 kutoka Sh104, Pembe Sh100 kutoka Sh106, huku Jogoo ikiuuza kilo hizo hizo mbili kwa Sh101 kutoka Sh105.

Serikali ya Kenya ina deni la Sh billioni 4 la wasagaji wa mahindi jambo lililowalazimisha wengi wao kupunguza kiwango cha mauzo na kuhodhi kiwango kikubwa cha akiba kwa ajili ya mau ya baadae.

” Kwa sasa tunanunua mahindi tunayotaka kuyasaga kwa siku na hatulimbikizi akiba kwasababu hatuna pesa za kutosha kwa hilo ,”alisema afisa wa chama cha wasagaji wa mahindi.

Kuongezeka kwa mauzo ya mahindi nchini Kenya kufuatia kiwango kikubwa cha bidhaa hiyo kuagizwa kutoka mataifa jirani ya Uganda na Tanzania .

Kenya ilisaini mkataba na seikali ya Uganda kununua magunia milioni 6.6 ya mahindi kwa gharama ya Sh2,050 kila mfuko ili kuziba pengo la uhaba wa magunia milioni tano uliosababishwa na hali mbaya ya hewa na kukabiliana na kupanda kwabei ya unga.

Unga wa Mahindi nchini Kenya hutumika kutengeneza Ugali ambao ni chakula kikuu kwa jamii nyingi nchini humo.

Kupanda kwa bei ya ”unga” kumekuwa kukisababisha mara kwa mara maandamano makubwa ya wananchi nchini Kenya wakilalamikia kuwa uhaba wake unasababisha maisha kuwa magumu majumbani mwao

Maandamano dhidi ya serikali yamekuwa yakishuhudiwa katika miaka iliyopita wananchi wakiilalamikia kwa kutochukua hatua za kudhibiti mapema mfumuko wa bei ya chakula hicho kinachopendwa sana nchini Kenya na mataifa mengine ya Afrika

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>