Published On: Thu, Apr 12th, 2018
World | Post by jerome

JESHI LA SYRIA LAHAMA KAMBI ZAKE KUHOFIA SHAMBULIO LA MAREKANI

Share This
Tags

Jeshi la Syria na washirika wake wamehama kutoka viwanja vya ndege na kambi za kijeshi nchini humo, pamoja na majengo ya Wizara ya Ulinzi na makao makuu ya jeshi Damascus, kwa hofu ya uwezekano wa mashambulizi ya Marekani.

Kundi la Hezbollah limewatuma saa 48 zilizopita wapiganaji wake walio nchini Syria tangu mwaka 2013 kupigana upande wa Jeshi la Syria wanaokadiriwa kuwa kati ya 5,000 na 8,000 nchini Syria.

Kundi hili la Kishia limehamisha wapiganaji wake kutoka ngome kambi zake na limeanza zoezi la kuweka sawa wapiganaji wake, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Kundi la Hezbollah na jeshi la Iran pia wamehamisha Askari wao kutoka ngome zao katika viwanja vidogo vya ndege vya kijeshi vya al-Chaayrate na T4, katika mkoa wa Homs, ambapo kulikua kukihifadhiwa ndege zisizokuwa na rubani.

Aprili 09 Mwaka huu Uwanja wa Ndege wa T4 ulishambuliwa kwa makombora, shambulizi ambalo liliua Askari kadhaa wa Iran na Syria na Mshirika wake Urusi walishtumu Israeli kuwa ilihusika na shambulizi hilo.

Hezbollah ilishiriki katika vita kabambe nchini Syria katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Kwa mujibu wa mashahidi kundi hilo lilipoteza wapiganaji 2,000 na 5,000 waliojeruhiwa nchini humo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>