Published On: Wed, Apr 4th, 2018

Hali ya ardhi ikizidi kuwa mbaya kutatishia maisha ya watu bilioni 3.2

Share This
Tags

Shirika la sera na sayansi kati ya serikali linalotoa huduma za hali ya kuwepo kwa aina nyingi za viumbe na mfumo wa kiviumbe IPBES ambalo linaungwa mkono na mashirika ya Umoja wa Mataifa limetoa ripoti ikisema shughuli za binadamu zimesababisha hali ya ardhi kuzidi kuwa mbaya, jambo ambalo linatishia maisha ya watu bilioni 3.2 duniani.

Ripoti hiyo imemalizika baada ya wataalamu zaidi ya 100 kutoka nchi 45 kufanya uchunguzi wa miaka mitatu. Ripoti hiyo inasema sababu ya moja kwa moja ni kupanuliwa kwa kasi kwa mashamba na maeneo ya malisho na usimamizi usiodumu wa ardhi, na sababu ya kimsingi ni njia ya maisha inayotumia rasilimali nyingi.

Ripoti hiyo inasema hadi mwaka 2014, zaidi ya hekta bilioni 1.5 ya ardhi ya asili imegeuzwa mashamba au malisho, eneo la ardhi ya asili lisiloathiriwa na shughuli za binadamu limekuwa chini ya robo moja ya nchi kavu duniani, na kiasi hiki kitaendelea kupungua na kuwa chini ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2050.

Mwandishi mmoja wa ripoti hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini Dr. Robert Scholes amesema katika miaka 30 ijayo, inakadiriwa kuwa watu bilioni 4 wataishi katika maeneo yenye ukame, watu milioni 50 hadi milioni 700 watalazimika kuhama, na kusababisha hali isiyo na utulivu kwenye jamii.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>