Published On: Fri, Apr 13th, 2018

CHANZO CHA WANYAMAPORI KUVAMIA MAKAZI YA WATU CHABAINIKA BUNGENI

Share This
Tags

Serikali imesema mabadiliko ya tabia ya Nchi na ongezeko la watu vimekua vikichangia Wanyamapori wakali na waharibifu kuingia katika makazi ya watu na kuharibu mali na kuleta madhara kwa binadamu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii JAFET HASUNGA, akijibu swali la mbunge wa Monduli JULIAS LAIZER amesema tatizo hilo lipo katika Wilaya zaidi ya 80 nchini.

Naibu waziri hasunga amesema hadi sasa serikali imeshalipa fidia ya kiasi cha shilingi milioni 48.01 ambazo zimelipwa kwa wananchi 251 wa Vijiji vya Wilaya ya Monduli waliokidhi vigezo vya kulipwa kuanzia mwaka 2010.

Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya rais TAMISEMI, Utumishi wa Umma na utawala bora wameitaka Serikali kutatu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ili kupandisha kiwango cha elimu nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>