Published On: Sat, Apr 21st, 2018

Buriani Masogange

Share This
Tags

Mwili wa Msanii AGNES GERALD Maarufu kwa jina la MASOGANGE unatarajiwa kuagwa kesho jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea Mkoani MBEYA Kwa maziko.

Mlimbwende huyo aliyekuwa na umri wa miaka 28 alinusurika kifungo cha miaka mwili baada ya hakimu wa mahakama ya Kisitu kumpata na hatia ya utumizi wa mihadarati.

Tarehe 6 Aprili hakimu mkaazi alimuagiza kulipa faini ya Tsh.1.5m la sivyo ahudumie kifungo cha miaka miwili.

Lakini mwezi Julai 2013 alikuwa miongoni mwa raia wawili wa Tanzania waliokamatwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini kwa madai ya kumiliki mihadarati.

Masogange alipata umaarufu 2010 wakati aliposhiriki katika kanda ya video ya wimbo wa msanii Belle9.

Kanda hiyo ya video ilijulikana kwa jina Masogange.

Alionekana katika kanda nyengine za video kabla ya kuwa mlimbwende aliyejiimarisha hatua iliompatia umaarufu mkubwa katika tasnia ya ulimwende wa kunogesha kanda za video nchini Tanzania.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>