Published On: Tue, Mar 13th, 2018

WAUZA MABONDO MWANZA WAIOMBA SERIKALI MUONGOZO WA VIPIMO

Share This
Tags

Umoja wa Wafanyabiashara wa Matumbo ya Samaki aina ya Sangara maarufu kama (Mabondo) Mkoani Mwanza wameiomba Serikali itoe muongozo wa vipimo sahihi juu ya ukubwa wa Mabondo na sheria ya uuzaji wa mabondo hayo.

Wafanyabiashara hao wanaamini muongoz huo rasmi utakawasaidia kufanya biashara hiyo kwa uhalali.

Wafanyabishara hao wamekutana ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakwamisha katika biashara zao ikiwemo kudai kuvamiwa katika Ofisi zao na kupigwa faini za mara kwa mara

Taasisi ya utafiti na udhibiti wa ubora wa Samaki EFTA mkaoni Mwanza ndiyo inayodai kuwa mabondo hayo yapo chini ya kiwango kinachotakiwa kuuzwa nje ya nchi .

Kutokana na changamoto hiyo baadhi ya Wafanyabishara wamefunga maduka yao na kushindwa kufanya biashara hiyo.

Baadhi ya Wafanyabishara wameeleza changamoto hiyo na kuiomba Serikali kutoa muongozo wa kipimo sahihi cha mabondo kinachotakiwa ili kiwasaidia wao kufanya biashara.

Juma Marco ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mabondo mkoani Mwanza, ameiomba Serikali kuliangalia suala hilo ili waweze kuendelea kufanya biashara hiyo ya Mabondo.

Ipo haja ya Serikali kukutana na wadau hao yaani Wafanyabishara wa Mabondo ili kuweka usawa wa jambo hilo na kutolea ufafanuzi kuhusu vipimo sahihi vya mabondo vinavyotakiwa na serikali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>