Published On: Tue, Mar 13th, 2018

TATIZO LA MAJI KWA WAKAZI WA WILAYA YA KOROGWE KUWA LA HISTORIA

Share This
Tags

Tatizo la maji kwa Wakazi wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga linatarajiwa kuwa historia baada ya Serikali kutoa Shilingi Milioni 500 za Mradi wa Maji.

Mbunge wa Korogwe mjini, Marry Chatanda, ameeleza Serikali imetoa fedha hizo zitakazosaidia Mradi wa Ujenzi wa Kisima hicho ili kukabiliana na tatizo la maji linalowakabili wananchi

Serikali wilayani humo imesema iko mbioni kukamilisha Mradi huo wa maji utakaokuwa mkombozi kwa wananchi hao.

Wakazi wa Kata ya Kilole wilayani humo wamesema walikuwa wakilazimika kunywa maji yenye vyura na ambayo si salama kwa Afya zao kutokana na shida ya maji kijijini hapo.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali Wilayani  Korogwe kupitia wataalam wake wamesema wako mbioni kukamilisha kisima cha maji chenye ujazo wa lita 225,000 ambapo zaidi ya wananchi 3,000 watafaidika na mradi huo.

Mradi huo wa Kisima cha Maji ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>