Published On: Sun, Mar 11th, 2018
World | Post by jerome

MSHINDI WA URAIS NCHINI SIERRA LEONE KUPATIKANA KATIKA DURU YA PILI

Share This
Tags

Dalili zinaonesha kuwa kutakuwa na duru ya pili nchini Sierra Leone kumpata rais mpya baada ya Tume ya Uchaguzi kuanza kutangaza matokeo ya awali siku ya Jumamosi.

Matokeo yanaonesha kuwa ushindani ni mkali sana kati ya mgombea wa chama tawala APC Samura Kamara yuko mbele kwa asilimia 43.2 dhidi ya mgombea wa upinzani wa chama cha SLPP Julius Maada Bio ambaye ana asilimia 43.09.

Sheria za Uchaguzi nchini humo zinaonesha kuwa mshindi anastahili kupata asimilia 55 ya kura zote zilizopigwa ili kutangazwa mshindi.

Wakati matokeo hayo ya awali yakitagazwa, wafuasi wa chama tawala na upinzani walikabiliana vikali jijini Freetown na kusababisha majeruhi huku wengine wakikamatwa.

Tume ya Uchaguzi imeomba uvumilivu wakati huu ikiendelea kujumuisha matokeo kabla ya kutangaza matokeo ya mwisho ambayo yanatarajiwa kufahamika wiki ijayo.

Duru ya pili kati ya mshindi wa kwanza na wa pili inatarajiwa kufanyika wiki mbili baada ya matokeo ya mwisho kutangazwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>