Published On: Tue, Mar 13th, 2018

MGOGORO WA KODI KATI YA WAFANYABIASHARA NA MANISPAA YA KIGOMA

Share This
Tags

Mgogoro wa kodi ya pango kati ya Wafanyabiashara na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, umeendelea kufukuta huku fungua funga ya mabanda katika soko la Mwanga na soko la Kigoma mjini nayo ikiendelea kuathiri shughuli za kiuchumi.

Ikiwa ni siku ya nane tangu Manispaa ya Kigoma Ujiji, kuyafunga mabanda hayo, wananchi ambao hutegemea masoko hayo kupata mahitaji mbali mbali, wameendelea kukosa huduma huku biashara nyingine kama ya boda boda na bidhaa za nafaka pia zikizorota.

Januari mwaka huu katika mkutano wa hadhara, Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe, walikuwa wamekubaliana katika vikao kushusha kiwango hicho cha kodi mpaka shilingi elfu 30 badala ya 50 iliyopitishwa, lakini wafanyabiashara waendelee kulipa elfu 50 wakati mchakato wa marekebisho ya sheria ukiendelea.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava, anaeleza hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuhusu kuzifanyia mabadiliko sheria hizo.

Wakati hayo yakiendelea wafanyabiashara nao wanasisitiza kwamba hawako tayari kulipa kodi ya pango ya shilingi 50,000, na kwamba kilio chao ni mbadiliko ya mapema ya sheria ndogo ili waweze kulipa shilingi elfu 30.

Katika jitihada za kumaliza mgogoro huo Chama cha Wafanyabiashara na Kilimo TCCIA, kimeomba kupewa muda wa mwezi mmoja wa kufanya utafiti ili kujua kiini cha mgogoro huo na waweze kushauri pande zote.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>