Published On: Tue, Mar 13th, 2018
World | Post by jerome

MCHEZA FILAMU ZA UTUPU STORMY DANIELS KUMSHTAKI RAIS DONALD TRUMP

Share This
Tags

Mcheza filamu za utupu Stormy Daniels, anamshtaki Rais Donald Trump kwa kile kinachoitwa ”hush agreement” ambayo ni makubaliano ya kutozungumzia mahusiano yao.

Daniels anadai kuwa yeye na Bwana Trump walikuwa na mahusiano tangu mwaka 2006, lakini alikana shutuma hizo.

Stormy Daniels alizaliwa Stephanie Clifford, Louisiana mwaka 1979.

Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu.

Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, ‘Storm’ na jina la kinywaji aina ya Whisky , ‘Jack Danniels’.

Unaweza kumtambua kwenye filamu ya ‘The 40-Year-Old Virgin’ na ‘Knocked Up’ na video ya muziki wa kundi la Maroon Five ‘Wake up call’

Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>