Published On: Tue, Mar 13th, 2018

JESHI LA POLISI NCHINI LAZITAKA KAMPUNI ZA ULINZI KUVAA SARE ZA AINA MOJA

Share This
Tags

Kampuni binafsi za ulinzi zinazoendesha shughuli zake hapa nchini zimetakiwa kuvaa sare za aina moja zilizokubaliwa na Jeshi la Polisi Tanzania.

Kampuni hizo zimetakiwa hadi kufikia Januari Mosi mwaka 2019 zinztakiwa zimwe zimetekeleza hatua hiyo, kwa lengo la kuondoa sare ambazo zimekuwa zikifanana na zinazovaliwa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Agizo hilo limetolewa Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii, Mussa Alli Mussa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kikao kilichowakutanisha Wamiliki wa Kampuni binafsi za ulinzi.

Kwa upande wao baadhi ya wamiliki wa Kampuni binafsi za ulinzi wamesema kuwepo kwa aina moja ya sare kutasaidia kuwatambulisha katika jamii na kufanya kazi zao kwa umakini zaidi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>