Published On: Mon, Mar 5th, 2018

JE VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO VINAPUNGUA TANZANIA?

Share This
Tags

Jumatano Februari 28, 2018 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alizindua ripoti ya makadirio ya watu nchini Tanzania inaonyesha ongezeko la watu kufikia watu milioni 54.2 huku ikikadiriwa idadi ya watu nchini Tanzania itafika takribani Milioni 77.5 ifikapo mwaka 2030

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ongezeko hilo linatokana (pamoja na sababu nyinginezo) uwepo wa idadi kubwa ya vizazi inayofikia milioni 2 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo inayotajwa kufikia 400,000 kwa mwaka lakini pia kupungua kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano

#CloudsCheck imefuatilia kwa kina suala la vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini ili kutaka kubaini kama kuna ongezeko au punguzo na mchango wake katika kuongezeka kwa idadi ya watu nchini.

Ripoti kadhaa za mashirika ya kimataifa zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano nchini.

Ripoti ya benki ya dunia (World Bank) inaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 nchini Tanzania. Ripoti hiyo inaonyesha kupungua kwa idadi ya vifo kutoka 179 kati ya kila watoto 1,000 mwaka 1990, kufikia 132 mwaka 2000, 72 mwaka 2010 hadi watoto 57 mwaka 2016

(Takwimu kwa mujibu wa benki ya Dunia)

Ripoti ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaonyesha pia kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania. Ripoti hiyo inaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya vifo kutoka 166 kati ya watoto 1,000 mwaka 1990 hadi kufikia 112 mwaka 2005 na 67 mwaka 2015

(Takwimu kwa mujibu wa UNICEF)

Kutokana na ripoti hizi, #CloudsCheck inahitimisha kuwa ni wazi kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano ni moja kati ya mambo yanayochangia kuongezeka kwa idadi ya watu nchini kama ilivyoelezwa katika ripoti ya makadirio ya watu nchini Tanzania. Hivyo NI KWELI kupungua kwa vifo kwa watoto chini ya miaka mitano nchini kunachangia kuongezeka kwa idadi ya watu nchini

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>