Published On: Tue, Mar 13th, 2018
Sports | Post by jerome

JE NI KWELI POLISI DAR ES SALAAM IMEPIGA MARUFUKU VIKUNDI “JOGGING” ?

Share This
Tags

Kumekuwepo na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikieleza kuwa kikosi cha usalama barabarani jijini Dar es Salaam kimepiga marufuku vikundi vyovyote vinavyoathiri matumizi ya barabara vikiwemo vile vinavyofanya mazoezi ya kukimbia “jogging”, kutumia barabara bila kupata kibali.

Taarifa hiyo inanukuu habari iliyoandikwa Jumanne tarehe 6 Februari 2018 na gazeti la habari leo ambalo lilifanya mahojiano ya ana kwa ana na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Marison Mwakyoma

#CloudsCheck imefanya ufuatiliaji wa kina ili kupata majibu sahihi ya nini hasa kikosi cha usalama barabarani kimeelekeza ikilenga kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa.

Watu wengi waliochangia mjadala huo katika mitandao ya kijamii wamehoji nini hasa lengo la kikosi hicho kuweka marufuku hiyo ambapo wengi wamegusia kwa kiasi kikubwa jitihada za makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu kuhamasisha jamii kufanya mazoezi. Mbali na kuhamasisha Makamu wa Rais ameshiriki mara kadhaa katika mazoezi huku akitangaza kila jumamosi ya pili ya mwezi kuwa siku maalum kwa mazoezi nchi nzima.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wametofautiana kwa kiasi kikubwa juu ya tamko hili ambapo upande mmoja wanaonyesha kuunga mkono wakisema mazoezi yafanyike katika viwanja vya wazi kwa utumizi wa barabara husababisha kuongezeka kwa foleni muda wa asubuhi katika siku za kufanya mazoezi huku upande mwingine ukipinga ambapo wanaeleza kuwa suala la kuweka utaratibu wa kutoa vibali ni usumbufu na litarudisha nyuma jitihada za kufanya mazoezi ambazo zimeshika kasi katika wilaya za jiji la Dar es Salaam

Baada ya sintofahamu hiyo  Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Marison Mwakyoma alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambapo alitoa ufafanuzi wa kina juu ya suala husika.

Alieleza kwa upana kuwa jeshi hilo halijapiga marufuku vikundi vinavyofanya mazoezi maarufu kama “jogging” lakini jeshi hilo liko katika mpango kabambe wa kupunguza na kumaliza  ajali na foleni jijini Dar es Salaam. Alifafanua kuwa baada ya kufanya tafiti waligundua sababu kadhaa zinazosababisha ajali na foleni ambapo mojawapo ni uwepo wa  vikundi vinavyofanya mazoezi ya kukimbia “jogging” hasa katika barabara kubwa “highway” akitolea mifano sehemu za Buguruni na Kurasini

Ameeleza kuwa kilichofanyika ni kuweka utaratibu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda usalama wa wale wanaofanya mazoezi. Akizungumza alinukuu kifungu cha 51 (12) cha sheria kinachoelekeza kutolewa kwa KIBALI pale kunapokuwepo na mwingiliano wa shughuli za watu na matumizi ya barabara

Hivyo ni wazi kuwa SI KWELI KWAMBA JESHI LA POLISI  LIMEKATAZA VIKUNDI VINAVYOFANYA MAZOEZI YA KUKIMBIA “JOGGING” bali limeweka utaratibu unaotaka kutolewa kwa “KIBALI” pale ambapo mazoezi yanafanyika katika barabara kubwa “Highway” lakini pia wametoa ushauri mazoezi yafanyike katika muda ambao hakuna magari mengi barabarani au yafanyike katika barabara ambazo hazina msongamano mkubwa wa magari.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>