Published On: Tue, Mar 13th, 2018
World | Post by jerome

JASUSI WA ZAMANI WA URUSI NA BINTI YAKE YABAINIKA WALIPEWA SUMU KALI

Share This
Tags

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, Jumatatu alisema jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake walipewa sumu kali ambayo ni sehemu ya kundi la kemikali za sumu kwa jina Novichok.

Sergei Skripal na binti yake Yulia bado wapo mahututi hospitalini kufuatia jaribio hilo la kuwaua eneo la Salisbury Machi mwaka huu.

Kemikali hiyo ilitambuliwa na Wataalamu katika maabara ya ulinzi na sayansi Porton Down.

Jina Novichok maana yake ni “mgeni” kwa lugha ya Kirusi.

Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.

Kemikali hizo ziliundwa na Muungano wa Usovieti miaka ya 1970 na 1980.

Zilifahamika kama silaha za kemikali za kizazi cha nne na zilistawishwa chini ya mpango wa silaha za Muungano wa Usovieti uliofahamika kama “Foliant”.

Mwaka 1999, maafisa wa ulinzi kutoka Marekani walisafiri hadi Uzbekistan kusaidia kuvunja na kusafisha moja ya eneo kubwa zaidi lililotumiwa kufanyia majaribio silaha za kemikali na Muungano wa Usovieti.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi za juu ambaye alitorokea Marekani, maafisa wa Usovieti walitumia kiwanda kilichokuwa eneo hilo kuunda na kufanyia majaribio sampuli za kemikali ya Novichok. Kemikali hii iliundwa mahsusi kutoweza kugunduliwa na wakaguzi wa silaha na sumu katika mataifa mengine.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>