Published On: Sun, Mar 11th, 2018

IGP SIRRO AAGIZWA KUWAKAMATA WATU WANAOPANGA MAANDAMANO

Share This
Tags

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amemuagiza na kumuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwakamata watu ambao wamepanga njama za kutaka kusababisha machafuko Nchini katika Maandamano ambayo yamezuiwa kuwa kinyume cha taratibu na sheria.

Mwigulu ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa salamu zake wakati wa Ziara ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli Mkoani Singida.

Rais Magufuli, amezindua kiwanda cha Alizeti Mkoani humo na kusema kinachotafutwa katika maandamano hayo ni namna ya watu wanatakanywa tawanywa ili kusudi waje kulalamika kuwa serikali ndio imeuwa watu wake.

Katika maagizo yake Waziri Mwigulu, amemuelekeza IGP Sirro wachukue hatua kwa wale watu wanaopanga mipango ya aina hiyo na kuchafua taswira ya nchi ama kwa mipango yao au ya wale wanaowatuma.

Waziri huyo wa mambo ya ndani ameongeza Watu wanataka mikusanyiko ili wafyatue na kuuwa watu  ili kuchafua taswira ya nchi yetu na tunayo mifano wa maeneo waliwahi kufanya jambo la aina hiyo na hatua zitachukuliwa”, amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema “Rais ndiyo maana unaona vinyago vinyago vingi hivi kama hivi juzi alitokea kijana mdogo amesema ametekwa, eti ametekwa na akapata muda wa kutafuta pafyumu na nguo za kubadilishia kule atakapokuwa ametekwa.

Unatowa wapi muda wa kujiandaa ?, watu wanatafuta njia za kuchafua taswira ya nchi yetu, na jambo hili Mhe. Rais kama ambavyo ulishatoa maelekezo, si jambo ambalo tutacheza nalo wala mjadala, hakuna sababu ya maandamano wala hakuna sehemu ya kuandamania na hakuna ruhusa ya kuandamana”.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>