Published On: Tue, Feb 27th, 2018
Business | Post by jerome

Wizara ya madini kuunda kamati kuchunguza mapato yatokanayo na uchimbaji wa dhahabu.

Share This
Tags

Wizara ya Madini nchini imelazimika kuunda kamati ya kuchunguza mapato yatokanayo na shughuli za uchimbaji  madini ya dhahabu kwenye maeneo iliyoyatoa kwa wachimbaji wadogo baada ya kubaini ufisadi unaofanywa na wamiliki wa vikundi vya uchimbaji kwenye  maeneo hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Nyakafuru Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita  kulalamika kuwa wanapunjwa mgawanyo wa  asilimia  kwa kile wanachokizalisha kwenye mashimo ya dhahabu.

Kufuatia malalamiko hayo Naibu Waziri wa madini Stansalaus Nyongo  ambaye amefanya ziara katika Mgodi wa Nyakafuru Wilaya  ya Mbogwe na  Mgodi wa   Bingwa Wilayani Geita, akalazimika kuunda kamati itakayokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya na Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita.

Pia Naibu Waziri huyo ametaka  kamati za ulinzi na usalama kwa Wilaya ya Mbogwe na Geita kuchunguza iwapo mapato  yatokanayo na madini ya dhahabu kwenye migodi hiyo kama  yanatumika ipasavyo au la katika shughuli za maendeleo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>