Published On: Wed, Feb 21st, 2018

Wizara ya afya yazindua kampeni maalum

Share This
Tags

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Thamini Uhai, wamezindua kampeni ya ‘Mjamzito na Mtoto Salama ni Wajibu Wetu’ yenye lengo la kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mchanga mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa utafiti wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuhusu idadi ya watu na afya Tanzania, ni asilimia 47 % tu ya wanawake mkoani Kigoma hujifungua katika vituo vya huduma za afya, hivyo kampeni hiyo inalenga kuhamasisha akina mama kwenda kujifungua katika vituo vya afya, kupanga na kujiandaa kujifungua.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga,ametaka kampeni hiyo kupewa umuhimu kuanzia katika mitaa na vitongoji ili iweze kuleta matokeo chanya.

Mkurugenzi wa Shirika la Thamini Uhai, Dkt.Nguke Mwakatundu, amesema kampeni ya miezi mitatu ya Mjamzito na Mtoto Salama, itahusisha matangazo ya redio ikiwemo CLOUDS FM, vipeperushi, mabango, uhamasishaji jamii na mawasiliano ya kibinafsi ili kueneza ujumbe muhimu.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka wizara ya afya, amesema tatizo la upatikanaji wa watoa huduma katika ngazi zote za huduma imekuwa ni changamoto kwa mikoa yote nchini lakini kwa mkoa wa Kigoma imekuwa ni changamoto kubwa sana.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>