Published On: Wed, Feb 7th, 2018
Sports | Post by jerome

Timu ya taifa ya Kenya kucheza na UAE katika mechi ya kwanza ya mashindano ya dunia nchini Namibia.

Share This
Tags

Timu ya taifa ya Kenya ya Mchezo wa Kriketi imewasili nchini Namibia kwa ajili ya kushiriki mashindano ya dunia kwa timu za daraja la pili ambako huko itashindana na timu za Nepal, Umoja wa Falme za Kiarabu, Canada, Oman na wenyeji Namibia.

Mashindano hayo licha ya kutoa bingwa, yatatumika kupata timu mbili zitakazokwenda kushiriki michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2019 nchini Zimbabwe kuanzia mwezi mechi 4 hadi 25.

Timu ambazo tayari zimeshapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kufuzu ni wenyeji Zimbabwe, Afghanistan, Papua New Guinea, Scotland, Uholanzi, Hong Kong, West Indies na Ireland.

Na washindi wa kwanza na washindi wa pili katika hizo zitaungana na timu 8 ambazo tayari zimefuzu michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Uingereza na Wales mwakani ambazo ni Uingereza, Australia, Bangladesh, India, New Zealand, Pakistan, South Africa na Sri Lanka.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>