Published On: Tue, Feb 20th, 2018
Business | Post by jerome

Serikali yaweka mikakati ya kumnufaisha mkulima wa kahawa

Share This
Tags

Serikali imeamua kufanya sensa ya wakulima wa zao la kahawa na mashamba yao ili kuweza kutambua kila mkulima ana uwezo wa kuzalisha kahawa kiasi gani kwa mwaka, lengo  likiwa ni  kukomesha biashara ya kinyonyaji ya Butura ambayo imekuwa ikitumiwa na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa.

Akiongea baada ya kutembelea mashamba ya wakulima wa kahawa na baadhi ya viwanda vya kukoboa kahawa katika mkoa wa Kagera,waziri wa kilimo na chakula Charles Tizeba, amesema serikali  imeamua kufanya sensa hiyo kwa wakulima ili kukomesha biashara ya  Butura  ambayo inatumiwa na baadhi ya wafanyabishara kwa kununua  kahawa ikiwa mashambani kwa bei ya chini ambayo haimnufaishi mkulima.

Tizeba amesema kahawa zote za wakulima zitauzwa kupitia vyama vyao vya msingi  lengo likiwa ni kuongeza bei ya kahawa na kuwafanya wakulima kunufaika na zao hilo.

Licha ya jitihada hizo zinazofanywa na serikali,wadau mbalimbali wanaojihusisha na biashara ya kahawa, wamesema biashara hiyo imegubikwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na halmashauri kutokuwa na maafisa ugani kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>