Published On: Wed, Feb 28th, 2018
Sports | Post by jerome

Rais Kenyatta aagiza kuanzishwa kwa programu za mafunzo ya mchezo wa gofu kwa shule za umma

Share This
Tags

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza kuanzishwa kwa mchezo wa gofu katika shule za umma kote nchini Kenya, kwa lengo la kuukuza na kufikia viwango vya kimataifa.

Uhuru Kenyatta ameyasema hayo wakati anakabidhi bendera ya taifa kwa timu ya taifa ya vijana inayokwenda kushiriki mashindano ya vijana nchini Morocco yanayoanza Machi 3 na kumalizika machi 10 mjini Cassablanca.

Kenya ni miongoni mwa mataifa 18 yanayoshiriki mashindano hayo ya Afrika kwa vijana yajulikanayo kama All Africa Junior Golf Championship.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>