Published On: Thu, Feb 8th, 2018
Sports | Post by jerome

Matokeo ya Ligi Kuu Soka Tanzania; Simba yaendelea kuongoza kwenye msimamo

Share This
Tags

Klabu ya soka ya Simba imeendelea kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania kufuatia ushindi wa 1-0 iliopta jana kwenye mechi dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Goli pekee la Simba limefungwa na mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi katika dakika ya 36 kutokana na pasi iliyotolewa na kiungo kutoka Ghana Asante Kwasi, na sasa timu hiyo inafikisha pointi 41 katika nafasi ya kwanza ikiwa ni tofauti ya pointi 7 dhidi ya Yanga wanaoshika nafasi ya pili.

Matokeo mengine katika mechi za ligi hiyo zilizopigwa jana, Mbao ikiwa nyumbani Mwanza imefungwa na Singida United magoli 2-1, Ndanda FC ya Mtwara imepata sare ya magoli 2-2 na Mbeya City, Mwadui ya Shinyanga imeifunga Mtibwa kwa magoli 3-1, Majimaji ya Ruvuma ikitoka sare ya bila Kufungana na Tanzania Prisons, na sare nyingine ya bila kufungana ikiwa ni baina ya Stand United na Lipuli kutoka Iringa Tanzania.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>