Published On: Thu, Feb 8th, 2018
Sports | Post by jerome

Makamu wa rais akutana na ujumbe wa Shimuta

Share This
Tags

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika  ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.

Akizungumza baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo  Khamis Mkanachi amesema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.

Pamoja na kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>