Published On: Tue, Feb 20th, 2018
Sports | Post by jerome

Baiskeli, Rwanda: Mashindano ya mataifa ya Afrika yazinduliwa jana mjini Kigali

Share This
Tags

Jumla ya waendesha baiskeli 167; 122 wanaume na 45 wanawake kutoka mataifa 22 tofauti wanashiriki mashindano ya Afrika yaliyofunguliwa jana mjini Kigali nchini Rwanda na yakitarajiwa kufikia tamati Februari 18.

Kwa mujibu wa Rais shirikisho la vyama vya mchezo ya baiskeli vya Afrika, Wagi Azzam, mashindano hayo ymegawanywa madaraja sita, kwa vijana wakiume na vijana wa kike, chini ya umri wa miaka 23, wanaume na wanawake na timu za wakubwa, wanaume kwa wanawake.

Hii ni mara ya pili kwa Rwanda kuandaa mashindano hayo katika kipindi cha miaka nane, lakini ikiwa haijawahi kupata medali ya dhahabu wala fedha.

Kutokana na umahiri ulioonyeshwa na waendesha baiskeli wa Rwanda tangu kuanza kwa mwaka huu chama cha baiskeli Rwanda kupitia Rais wake kimewaahidi mashabiki kuwa safari hii ubingwa utabaki Kigali hivyo wajitokeze kwa wingi.

Pamoja na mabingwa watetezi, timu ya taifa ya Eritrea timu zingine zinazoshiriki ni Algeria, Morocco, Afrika Kusini, Nigeria, Swaziland, Shelisheli, Namibia, Djibouti, Mauritius, Benin, Kenya, Burkina Faso, Ghana, Zambia, Sudan, Uganda, DRC, Misri na Burundi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>