Published On: Wed, Jan 31st, 2018

Watumishi 16 wa sekta ya ardhi wafukuzwa kazi.

Share This
Tags

Watumishi 16 wa sekta ya ardhi wamefukuzwa kazi huku watumishi 19 waliopo chini ya wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakipewa onyo kwa makosa mbalimbli  yanayochochea migogoro ya ardhi nchini kati ya mwaka 2014 hadi 2017.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ANGELINA MABULA ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora mjini EMMANUEL MWAKASAKA aliyeuliza hatua za serikali kutatua migogoro ya arhi nchini huku chanzo kikiwa ni maafisa ardhi.

MABULA amesema kwa watumishi wa ardhi waliopo chini ya mamlaka ya serikali za mitaa, wizara hiyo imekuwa ikishirikiana na TAMISEMI kuhakikisha wanaobainika kutenda makosa wanachukuliwa hatua stahiki.

Katika hatua nyingine serikali imesema itazungumza na wafanyabiashara wa mafuta ili kuangalia tozo ambazo ni kero kwa wazanzibari.

Naibu waziri uchukuzi na mawasiliano mhandisi  ATASHASTA NDITIYE akijibu swali la mbunge wa baraza la wawakilishi JAKU HASHIM AYOUB amesema Tanzania bara na Zanzibar ni nchi moja hivyo shehena inayoenda Zanzibar  tozo yake ni sawa na sehemu nyingine nchini.

Pia serikali imewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika program zake ili kutokomeza tatizo la watoto kupotea mkoani Dar es salam ambapo kwa mwaka 2017 watoto 184 walipotea.

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi HAMAD MASAUNI akijibu swali la mbunge wa viti maalum FAHARIA SHOMARI, amesema ili kukabiliana na tatizo hilo la kupotea kwa watoto, serikali kupitia jeshi la polisi imeanzisha mfumo wa polisi jamii mashuleni.

Bunge limepokea na kujadili muswada wa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma wa mwaka 2018.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>