Published On: Wed, Jan 31st, 2018
Business | Post by jerome

Wananchi wa Kilolo washauriwa kulima korosho

Share This
Tags

Wananchi wa kijiji cha nyamagana kata ya mahenge wilayani kilolo mkoani Iringa wametakiwa kulima zao la  korosho ili kujikwamua kiuchumi kutokana na kuwepo soko la uhakika la zao hilo badala ya kutegemea kilimo cha mahindi na vitunguu pekee.

Idadi kubwa ya wakazi wa nyamagana hutegemea shuguli ya kilimo cha mahindi na vitunguu  ilhali mazao hayo yakiwa ni ya msimu, tofauti na kilimo cha korosho.

Kauli  hiyo imeolewa na mkuu wa wilaya ya kilolo asia abdallah wakati wa uzinduzi wa zao hilo kijijini hapo ambapo amewataka wananchi hao kujikita katika zao la korosho kutokana na uwepo wa soko la uhakika.

Kwa mujibu wa afisa kilimo wa wilaya ya kilolo,  mpaka sasa wamezalisha zaidi ya miche ya korosho 45,000 huku kila hekari moja ikichukua miche 30 pekee.​

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>