Published On: Tue, Jan 16th, 2018

Utafiti waonesha hali ya usingizi kwa wafanyakazi wa ofisini si nzuri

Share This
Tags

Utafiti mpya uliofanywa na mtandao wa kijamii wa China umeonesha kuwa hali ya usingizi wa wafanyakazi wa ofisini si nzuri, hasa wafanyakazi wanaopanga nyumba moja, ambao asilimia 20 kati yao wanalala baada ya saa saba usiku.

Utafiti huo umeonesha kuwa wafanyakazi wengi wanalala kati ya saa nne hadi sita usiku, na baadhi yao wanachelewa zaidi kulala. VSababu kuu ya kuwachelewesha kulala ni matumizi ya mtandao wa Internet, kucheza game, kuchat na mambo mengine, tabia ya kuchelewa kulala na zamu ya usiku. Zaidi ya asilimia 55 ya wafanyakazi waliohojiwa wamesema, kutumia mtandao wa kijamii, kusoma forum na kununua bidhaa kwenye mtandao wa internet ni jambo la lazima kabla ya kulala. Mbali na hayo, kiwango cha watu wanaochelewa kulala kutokana na kucheza game kimechukua asilimia 25.

Utaifi huo pia umesema, licha ya sababu tano zilizotajwa, bado kuna sababu zinazoshangaza watu. Asilimia 17 ya watu waliohojiwa wamesema, wanachelewa kulala kutokana na kufikiria maisha ya siku za baadaye.

Wataalamu wamependekeza kuwa kujenga tabia ya kulala na kuamka mapema ni muhimu sana, mazingira mazuri pia yanasaidia usingizi bora.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>