Published On: Wed, Jan 31st, 2018

Serikali kuwachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika

Share This
Tags

Waziri wa kilimo Dk. CHARLES TIZEBA, amesema jamii imechoshwa na vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika nchini na wale wanaoendelea kufanya hivyo kwa kusaini mikataba mibovu watachukuliwa hatua stahiki pale watakapobainika kusababisha hasara.

 

TIZEBA amesema hayo mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya baraza la makamishna wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini na kuwaasa makamishna hao kuhakikisha heshima ya ushirika inarejea

 

Amesema kwa sasa jamii imeanza kuanzisha vikundi mbalimbali vya ushirikiano lakini vinaogopa kutumia neno ushirika kwa kuwa heshima ya jina hilo kwa jamii limeshuka.

  

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo Dk. Titus Kamani amesema wanatambua kuwa heshima ya ushirika nchini imeshuka lakini wao kwa nafasi yao ya ukamishna wa tume ya maendeleo ya ushirika watahakikisha wanarejesha heshima iliyopotea.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>