Published On: Wed, Jan 10th, 2018

Picha ya mvulana iliyowaweka taabani H&M

Share This
Tags

Wasanii na wachezaji mashuhuri duniani wamekosoa hatua ya kampuni ya mavazi na mitindo ya H&M kuweka tangazo la mvulana mweusi akiwa amevalia fulana yenye ujumbe ambao umefasiriwa kuwa wa ubaguzi wa rangi.

Fulana hiyo ya rangi ya kijani ilikuwa na ujumbe “coolest monkey in the jungle“, kwa maana ya tumbili mtanashati au bora zaidi porini.

Mwanamuziki Diddy na mchezaji wa Manchester United Romelu Lukaku wamechukua hatua ya kupakia picha zenye ujumbe mbadala.

Mwanamuziki Abel Makkonen Tesfaye, maarufu kama The Weeknd, amesema hatafanya kazi tena na kampuni ya mavazi na mitindo ya H&M baada ya tangazo hilo.

The Weeknd amesema tangazo hilo limemuacha na “mshangao na aibu kubwa”.

Mwanamuziki huyo awali amewahi kuuza bidhaa zenye nembo yake kupitia H&M na pia kuwatangazia bidhaa zao.

Ameandika kwenye Twitter kwamba amekerwa sana na picha hiyo.

H&M wamesema: “Tunasikitika sana kwamba picha hiyo ilipigwa, na tunajutia sana kwamba ilisambazwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>