Published On: Wed, Jan 10th, 2018
Science | Post by jerome

Mwanasayansi wa Japan aomba msamaha kwa kudanganya kukua sentimita 9 akiwa angani

Share This
Tags

Mwanasayansi wa anga za juu wa Japan ameomba msamaha kwa kusema kimakosa kuwa alikuwa amekuwa kwa sentimita 9 tangu awasili kwenye kituo cha kimataifa cha anga za juu (ISS) wiki tatu zilizopita.

Norishige Kanai alisema kwa hakika alikuwa amekuwa kwa sentimita mbili akilaumu kasoro ya vipimo.

“Ninaomba msamaha kwa kuandika habari za uongo kama hizo,” aliandika kwa lugha ya kijapani.

Madai yake ya awali ya uongo yalizua maoni miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wanasayansi kwa kawaida hukua kwa takriban sentimita 2-5 wanapokuwa katika kituo cha anga za juu.

Bw. Kanai awalia alikuwa ameandika kwa lugha ya kijapani akisema, “Habari za asubuhi nyote, nina tangazo muhimu kwa kila mtu. Tulimpimwa miili yutu baada ya kufika angani na wao, wao, wao, nimekua kwa sentimita 9!

“Nimekua kama mmea kwa wiki tatu tu. Kitu kama hiki hakijafanyika tangu nilipokuwa shule ya upili. Nina hofu ikiwa nitatoshea kwenye chombo cha Soyuz wakati nitarudi duniani.

Chombo cha Soyuz kinachowasafirisha wanasayansi kwenda angani na kurudi kina vipimo vya urefu wa kuketi na ikiwa mtu atakuwa mrefu zaidi itakuwa ni tatizo kubwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>