Published On: Wed, Jan 31st, 2018

Mpango wa TASAF waingiwa na Dosari Bukoba

Share This
Tags

Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF katika wilaya ya Bukoba umeingiwa dosari baada ya watendaji wanaogawa pesa kwa walengwa kuwatoza shilling elfu moja kwa kila mmoja apokeapo fedha hizo,suala ambalo linaelezwa kuwa ni kinyume na utaratibu wa mpango huo.

Licha ya mpango huo kuwa mkombozi kwa kaya zinazoendelea kunufaika, baadhi ya wananchi wamewalalamikia watendaji wanaohusika katika zoezi la ugawaji wa fedha hizo kwa kuwakata pesa zao..

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo wa TASAF kwa Katibu wa siasa  na ushirikiano wa mambo ya nje wa chama cha mapinduzi CCM aliyetembelea baadhi ya Kaya zinazonufaika na mpango huo,mkuu wa wilaya ya Bukoba  Deodatus Kinawilo amesema zipo dosari na  malalamishi kutoka kwa walengwa na wanaendelea kuyatafutia ufumbuzi.

Akiongea baada ya kutembelea baadhi ya kaya zinazonufaika na mpango wa TASAF Katibu huyo wa siasa  na ushirikiano wa mambo ya nje wa chama cha mapinduzi CCM, NGEMELA LUBINGA amesema malengo ya serikali kuanzisha mpango huo ni kuwawezesha wananchi waondokane na umasikini.

Zaidi ya shilingi bilioni 6.5 zimeshatolewa na serikali na tayari kaya zaidi ya elfu 11 zimenufaika na mpango huo toka Julai 2015 hadi December  2017 katika wilaya ya Bukoba.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>